Эсперанта-суахілі кніга-білінгва
Ni, anoj de la tutmonda movado por la progresigo de esperanto, direktas ĉi tiun manifeston al ĉiuj registaroj, internaciaj organizoj kaj homoj de bona volo, deklaras nian intencon firmvole plulabori por la celoj ĉi tie esprimitaj, kaj invitas ĉiun unuopan organizaĵon kaj homon aliĝi al nia strebado.
Sisi, wanachama wa chama cha kimataifa cha maendeleo ya Kiesperanto, tunatoa tangazo hilo kwa serikali zote, vyombo vyote vya kimataifa na binadamu wote wenye nia njema, tunatangaza nia yetu kuendelea kwa bidii kukidhi madhumuni yaelezwayo hapa chini tukiita kila chama na kila mtu waungane nasi katika juhudi zetu.
Lanĉita en 1887 kiel projekto de helplingvo por internacia komunikado, kaj rapide evoluinta en vivoplenan, nuancoriĉan lingvon, esperanto jam de pli ol jarcento funkcias por kunligi homojn trans lingvaj kaj kulturaj baroj. Intertempe la celoj de ĝiaj parolantoj ne perdis gravecon kaj aktualecon. Nek la tutmonda uzado de kelkaj lingvoj, nek progresoj en la komunikad-tekniko, nek la malkovro de novaj metodoj de lingvo-instruado verŝajne realigos jenajn principojn, kiujn ni konsideras esencaj por justa kaj efika lingva ordo.
Tangu zaidi ya karne moja Kiesperanto, kilichoanzishwa mnamo 1887 kama mpango wa lugha kisaidizi katika mawasiliano ya kimataifa na kilichogeuka upesi kuwa lugha yenye maana nyingi na uhai wa peke yake, ni njia ya kuunganisha watu kupita migogoro ya kilugha na ya kiutamaduni. Wakati huo huo madhumuni ya Kiesperanto hayajakosa maana na muhimu. Wala utumizi wa lugha kadhaa za kitaifa katika dunia nzima wala maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano, wala ustawi wa mbinu mpya za fundisho la lugha hazitatekeleza mfumo wa kilugha ulio sawa na wa kufaa unaotegemea kanuni zifuatazo na tunazozihesabia za lazima.
1. Demokratio
1. Demokrasia
Komunika sistemo, kiu tutvive privilegias iujn homojn, sed postulas de aliaj, ke ili investu jarojn da penoj por atingi malpli altan gradon de kapablo, estas fundamente maldemokratia. Kvankam, kiel ĉiu lingvo, esperanto ne estas perfekta, ĝi ege superas ĉiun rivalon en la sfero de egaleca tutmonda komunikado.
Kila mfumo wa mawasiliano unaowapendelea watu wachache daima, huku unawalazimisha wengine watoe miaka ya juhudi ili wapate kiwango cha chini cha umahiri (ufasaha na usahihi) ni kinyume kabisa cha usawa. Ingawa Kiesperanto, kama lugha yoyote, si kamilifu, kinapita kabisa kwa usawa lugha zote zitumikazo kwa mawasiliano popote duniani.
Ni asertas, ke lingva malegaleco sekvigas komunikan malegalecon je ĉiuj niveloj, inkluzive de la internacia nivelo. Ni estas movado por demokratia komunikado.
Sisi tunathibitisha kwamba ukosefu wa usawa wa kilugha unazaa ukosefu wa usawa wa kimawasiliano katika viwango vyote, pamoja na kiwango cha kimataifa. Sisi ni ushirikiano unaotaka mawasiliano yenye usawa.
2. Transnacia edukado
2. Elimu ya kimataifa
Ĉiu etna lingvo estas ligita al difinita kulturo kaj naci(ar)o. Ekzemple, la lernejano, kiu studas la anglan, lernas pri la kulturo, geografio kaj politiko de la anglalingvaj landoj, precipe Usono kaj Britio. La lernejano, kiu studas esperanton, lernas pri la mondo sen limoj, en kiu ĉiu lando prezentiĝas kiel hejmo.
Kila lugha ya kitaifa inaungana na utamaduni fulani na taifa au mataifa fulani. Kwa mfano, mwanafunzi anayesoma Kiingereza anafundishwa utamaduni, jiografia na mifumo ya kisiasa za mataifa yanayotumia Kiingereza, hasa Marekani na Uingereza. Mwanafunzi anayesoma Kiesperanto anafundishwa kuhusu dunia bila mipaka, ambapo taifa yo yote si ngeni kwake.
Ni asertas, ke la edukado per iu ajn etna lingvo estas ligita al difinita perspektivo pri la mondo. Ni estas movado de transnacia edukado.
Sisi tunathibitisha kwamba elimu ikitekelea kwa njia ya lugha yoyote ya kitaifa imeungana na maoni fulani ya ulimwengu. Sisi ni ushirikiano unaotaka elimu ya kimataifa.
3. Pedagogia efikeco
3. Manufaa ya kimafunzo
Nur malgranda procentaĵo el tiuj, kiuj studas fremdan lingvon, ekmastras ĝin. Plena posedo de esperanto eblas eĉ per memstudado. Diversaj studoj raportis propedeŭtikajn efikojn al la lernado de aliaj lingvoj. Oni ankaŭ rekomendas esperanton kiel kernan eron en kursoj por la lingva konsciigo de lernantoj.
Asilimia chache tu ya wanafunzi wa lugha ngeni wanafikia umahiri wa lugha lengwa hiyo. Umahiri wa Kiesperanto unafikiwa hata kwa masomo ya kitabuni. Utafiti umeonyesha kwamba Kiesperanto inafaa kama andalio la masomo ya lugha zingine. Tena, kimependekezwa kama sehemu ya maana hasa katika masomo ya utambuzi wa kilugha.
Ni asertas, ke la malfacileco de la etnaj lingvoj ĉiam prezentos obstaklon por multaj lernantoj, kiuj tamen profitus el la scio de dua lingvo. Ni estas movado por efika lingvo-instruado.
Sisi tunathibitisha kwamba matatizo katika ujifunzaji wa lugha za kitaifa yatakuwa daima kikwazo kwa wanafunzi wengi ambao wangefaidi kutoka ujuaji wa lugha ya pili. Sisi ni ushirikiano unaotaka kuendeleza ujifunzaji halisi wa lugha.
4. Plurlingveco
4. Ulumbi
La esperanto-komunumo estas unu el malmultaj mondskalaj lingvokomunumoj, kies parolantoj estas senescepte du- aŭ plurlingvaj. Ĉiu komunumano akceptis la taskon lerni almenaŭ unu fremdan lingvon ĝis parola grado. Multokaze tio kondukas al la scio de kaj amo al pluraj lingvoj, kaj ĝenerale al pli vasta persona horizonto.
Jamii ya Kiesperanto karibu haina kifani kama jamii ieneayo popote duniani: watumizi wake wajua lugha mbili au zaidi. Kila mwanajamii amejitihadi kujifunza angalau lugha ngeni moja kufikia kiwango cha kuwasiliana. Nyakati nyingi hicho kinaelekea kuzipenda na kuzijua lugha nyingi na kwa jumla kupanua fikira zake mwenyewe.
Ni asertas, ke la anoj de ĉiuj lingvoj, grandaj kaj malgrandaj, devus disponi pri reala ŝanco por alproprigi duan lingvon ĝis alta komunika nivelo. Ni estas movado por la provizo de tiu ŝanco.
Sisi tunathibitisha kwamba watumizi wa kila lugha, kubwa au ndogo, lazima wawe na nafasi ya kweli ya kusoma lugha ya pili kufikia kiwango cha juu cha kimawasiliano. Sisi ni ushirikiano unaotaka kuwapa wote fursa hiyo.
5. Lingvaj rajtoj
5. Haki za lugha
La malegala disdivido de potenco inter la lingvoj estas recepto por konstanta lingva malsekureco, aŭ rekta lingva subpremado ĉe granda parto de la monda loĝantaro. En la esperanto-komunumo la anoj de lingvoj grandaj kaj malgrandaj, oficialaj kaj neoficialaj, kunvenas sur neŭtrala tereno, dank' al la reciproka volo kompromisi. Tia ekvilibro inter lingvaj rajtoj kaj respondecoj liveras precedencon por evoluigi kaj pritaksi aliajn solvojn al la lingva malegaleco kaj lingvaj konfliktoj.
Ugawanyaji wa uwezo usio sawa kati ya lugha ni chanzo cha mashaka ya kilugha ya daima, au udhalimu dhahiri wa kilugha, kwa baadhi kubwa ya binadamu. Katika jamii ya Kiesperanto watumizi wa lugha kubwa na dogo, iliyo au isiyo rasmi wanakutana katika usawa kwa sababu ya mapatano ya kuridhiana. Usawa huo wa haki za lugha na madaraka unatoa msingi wa ustawishaji na uchunguzi wa matatuzi mengine ya utofauti na mpambano wa lugha.
Ni asertas, ke la vastaj potencodiferencoj inter la lingvoj subfosas la garantiojn esprimitajn en tiom da internaciaj dokumentoj, de egaleca traktado sendistinge pri la lingvo. Ni estas movado por lingvaj rajtoj.
Sisi tunathibitisha kwamba tofauti kubwa za uwezo baina ya lugha zinadhoofisha hakika, inayotajwa katika vyombo vingi vya kimataifa, ya usawa bila kujali lugha. Sisi ni ushirikiano unaopigania haki za lugha.
6. Lingva diverseco
6. Utofauti wa lugha
La naciaj registaroj emas konsideri la grandan diversecon de lingvoj en la mondo kiel baron al komunikado kaj evoluigo. Por la esperanto-komunumo, tamen, la lingva diverseco estas konstanta kaj nemalhavebla fonto de riĉeco. Sekve, ĉiu lingvo, kiel ĉiu vivaĵospecio, estas valora jam pro si mem kaj inda je protektado kaj subtenado.
Serikali za kitaifa zinaelekea kuhesabia utofauti mkubwa wa lugha duniani kama kikwazo cha mawasiliano na maendeleo. Katika jamii ya Kiesperanto, walakini, utofauti wa lugha unafikirika chanzo thabiti na cha lazima cha ustawishaji. Kwa sababu hiyo kila lugha, kama viumbehai vyote, asili yake ni ya thamani na inastahiki ulinzi na msaada.
Ni asertas, ke la politiko de komunikado kaj evoluigo, se ĝi ne estas bazita sur respekto al kaj subteno de ĉiuj lingvoj, kondamnas al formorto la plimulton de la lingvoj de la mondo. Ni estas movado por lingva diverseco.
Sisi tunathibitisha kwamba sera za mawasiliano na maendeleo zisizotegemea heshima na msaada kwa kila lugha zinazihukumu wingi wa lugha za dunia ziuawe. Sisi ni ushirikiano unaothamini utofauti wa lugha.
7. Homa emancipiĝo
7. Uhuru wa binadamu
Ĉiu lingvo liberigas kaj malliberigas siajn anojn, donante al ili la povon komuniki inter si, barante la komunikadon kun aliaj. Planita kiel universala komunikilo, esperanto estas unu el la grandaj funkciantaj projektoj de la homa emancipiĝo — projekto por ebligi al ĉiu homo partopreni kiel individuo en la homa komunumo, kun firmaj radikoj ĉe sia loka kultura kaj lingva identeco, sed ne limigite de ili.
Kila lugha inafungua na inafunga watumizi wake kwa kuwapa ubingwa wa kuwasiliana baina yao lakini inazuia mawasiliano na wasemaji wa lugha nyingine. Kiesperanto, kilichopangwa kama njia ya mawasiliano ya watu wote, ni mmojawapo wa mipango mikubwa inayofaa kwa ukombozi wa binadamu — kinachokusudia kumwezesha kila raia ashiriki kabisa jamii ya binadamu, akiwa na shina imara ndani ya utamaduni na lugha yake, lakini asizuiwe nayo.
Ni asertas, ke la ekskluziva uzado de naciaj lingvoj neeviteble starigas barojn al la liberecoj de sinesprimado, komunikado kaj asociiĝo. Ni estas movado por la homa emancipiĝo.
Sisi tunathibitisha kwamba bila shaka kutumia lugha za kitaifa tu kunaweka vikwazo vya uhuru wa kusema, kuwasiliana na kushirikiana. Sisi ni ushirikiano unaopigania uhuru wa binadamu.
Prago, jul. 1996
Prago, jul. 1996
Рэклама